Francesco Spinelli (Milano, 14 Aprili 1853 – Rivolta d'Adda, 6 Februari 1913[1]) alikuwa padri wa Kanisa Katoliki kutoka Italia Kaskazini.
Alianzisha na kuongoza kati ya matatizo mengine shirika la kitawa la Masista Waabuduo Sakramenti Takatifu Sana (1882) ambalo baadaye liligawanyika (1892), akivumilia yote kwa ajili ya Mungu[2].
Alitangazwa mwenye heri na Papa Yohane Paulo II 21 Juni 1992, halafu mtakatifu na Papa Fransisko tarehe 14 Oktoba 2018.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[3].